Alhamisi , 5th Nov , 2015

Uwekaji wa Nyasi bandia katika uwanja wa Kaitaba wa mjini Bukoba unatarajia kukamilika ndani ya siku 14 ili uweze kutumika.

Katibu wa chama cha soka mkoa wa Kagera KRFA Salum Chama amesema, iwapo hakutakuwa na mvua kali uwekaji wa nyasi hizo utakamilika ndani ya siku zilizopangwa.

Chama amesema, uwanja huo utakuwa bora kuliko awali maana nyasi hizo zitafanya kuwa kiwanja cha kisasa na kuongeza mapato kwa mkoa wa Kagera na klabu ya Kagera Sugar ambao ndiyo watumiaji wa uwanja huo.

Uwekaji wa nyasi bandia ulianza Agosti mwaka jana ambapo pia ulifungwa msimu uliopita wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwa lengo la kupisha uwekaji wa nyasi hizo.