Meddie Kagere akishangilia bao kwa staili ya kufunga jicho, kulia kwake ni kiungo Hassan Dilunga akijumuika nae kumpongeza.
Kagere hakua katika kiwango bora tangu kurejea kwa msimu baada ya Covid-19,lakini ameanza kurejesha makali yake kwa kufunga mechi ya pili mfululizo baada ya kufanya kama hivyo uliopita dhidi ya Mbao kufunga licha ya Simba kupoteza kwa bao 3-2.
.
Matamanio ya wengi Ni kushuhudia Kagere anaivunja rekodi ya aliyekua mshambuliaji wa Yanga, Mohamed Hussein Machinga aliyoiweka mwaka 1999 ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ndani ya msimu mmoja ambapo alipachika mabao 26.
.
Nyota aliyekaribia rekodi hiyo ya Machinga ni Abdallah Juma ambaye akiwa na Mtibwa Sugar mwaka 2006 alifunga mabao 25 ndani ya msimu lakini akashindwa kuifikia rekodi ya mabao 26 iliyowekwa na Mohamed Hussein..
.
Iwapo Kagere raia wa Rwanda atahitaji kuweka rekodi yake katika ligi kuu itambidi afunge mabao matano ndani ya mechi mbili zilizosalia katika ligi kuu Tanzania bara.
Hadi sasa nyota huyo wa Rwanda amefunga mabao 22, na kabakisha bao moja afikie idadi ya mabao aliyofungwa mwaka jana huku akiwa ametoa pasi 8 za usaidizi zilizozaa mabao.




