Ijumaa , 24th Jul , 2020

Juventus imechemsha kutwaa ubingwa wa Serie A mapema baada ya kufungwa 2-1 na Udinese kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia.

Juventus inahitaji kushinda mechi 1 kati ya 3 kutawaa ubigwa wa Serie A

Juventus imechemsha kutwaa ubingwa wa Serie A mapema baada ya kufungwa 2-1 na Udinese kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia.

Endapo Juve ingeshinda mchezo huo, ingekuwa inachukua ubingwa wa Serie A kwa mara ya tisa mfululizo.

Juve wanaweza kutwaa taji hilo katika ushindi wa mechi moja kati ya tatu zilizobaki, lakini hivi karibuni wameshuka kiwango.

Wameshinda mechi moja tu katika michezo mitano ya Serie A, lakini wana unafuu kutokana na timu tatu za chini yao, Atalanta, Inter Milan na Lazio wamepoteza michezo yao ya hivi karibuni.

IMMOBILE AMPA WAKATI MGUMU RONALDO

Cristiano Ronaldo amepitwa goli moja na mshambuliaji wa Lazio Ciro Immobile katika mbio za kugombea kiatu cha dhahabu.

Immobile alifunga bao lake la 31 la msimu katika ushindi wa Lazio wa 2-1 dhidi ya Cagliari.