Juma Abdul
Yanga watacheza dhidi ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation (FA), utakaofanyika Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Juma Abdul amesema timu hiyo inaendelea kujipanga kikamilifu kuwakabili Simba na kuwataka mashabiki wa Yanga waache kuwasikiliza wapinzani wao, kwani mbinu wanazopewa kwa sasa zinalenga kwenda kupata ushindi.
"Mashabiki wa Simba wanaongea kiasi kwamba mashabiki wetu wameanza kurudi nyuma, niwaombe waendelee kuwa na furaha kwenye kipindi hiki kwani ubora wa kikosi cha Simba tunaujua na mbinu anazotupa mwalimu zinalenga kwenda kumaliza mchezo ndani ya dakika 90," alisema Abdul

