Ijumaa , 16th Sep , 2022

Promota wa bondia Mwingereza Anthony Joshua Eddie Hearn amesema haoni kama kuna vizingiti vitakavyo sababisha pambano la uzito wa juu kati ya  Anthony Joshua na Tyson Fury kutofanyika, amesisitiza kuwa Joshua anataka pambano lifanyike.

"Joshua alihisi pambano hili litapotea ikiwa halitafanyika sasa na kukubaliana na mkataba wa Fury. Tuna uhakika mkataba utakuwa nasi siku moja au mbili zijazo. Maadamu unaakisi ofa ya Tyson  ambayo Warrens (Promota  wa Tyson Fury) anasema inafanya  pambano hilo lifanyike. Tumeambiwa Tyson Fury analitaka sanaa  hili pambano kama Joshua anavyo litaka." Amesema Eddie Hearn

Mabondia hawa wawili kutoka Uingereza kwenye makubaliano ya awali wamekubaliana pambao hilo la kumaliza utata yupi ni mbabe wa masumbwi katika taifa hilo lifanyike Disemba 3, 2022. Pambano hili litakuwa la kuwania mkanda wa uzito wa juu wa WBC ambao kwa sasa anauhikilia Tyson Fury.