Baada ya kupokea matibabu, alionyesha kutoweza kuendelea na mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Mateo Kovacic, hali iliyozua hofu miongoni mwa mashabiki wa City kuhusu uzito wa jeraha hilo.
Mtaalamu wa majeraha wa Manchester City, alionesha tathmini yenye wasiwasi kwenye ukurasa wa Twitter, akieleza kwamba Rodri anaweza kuwa na jeraha katika goti lake la kulia kutokana na jinsi goti lake lilivyohama wakati wa mgongano hio.
alisema. Katika mazungumzoi baada ya mechi, meneja wa City, Pep Guardiola, alikiri nguvu za Rodri na kusema kwamba mchezaji huyo aliondoka uwanjani kwa sababu alihisi kuna tatizo.
Ripoti mbali mbali zinaeleza kuwa jeraha hilo limethibitishwa kuwa ni jeraha la ligament ya anterior cruciate (ACL), na atakaa nje ya msimu mpaka taarifa ya kupona kwake itakapotolewa na jopo la matabibu wa klabu ya Manchester City.