Jumatatu , 25th Jan , 2016

Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefuzu robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani baada ya kuinyuka Gabon mabao 4-1 kwenye mchezo wa kundi A uliopigwa jana nchini Rwanda.

Michuano ya CHAN 2016 nchini RWANDA

Mabao ya Ivory Coast yalifungwa na Aka Essis, Djedje Guiza, Koffi Boua na Nilmar Ble na lile la La gabon lilifungwa na Franck Obambou.

Ivory Coast inaungana na Rwanda ambayo imemaliza kama kinara wa kundi hilo licha ya jana kuchezea kipigo cha bao 4-1 kutoka kwa Morocco lakini wao waliifunga bao 1-0 Ivory Coast kwenye mechi ya kwanza ya kundi hilo.

Hii leo kutapigwa mechi za mwisho za Kundi B ambapo Ethiopia itaumana na Angola huku Cameroon ikiumana na Congo DR ambayo imeshafuzu hatua ya robo fainali.