Jumamosi , 25th Jul , 2020

Mkataba wa Messi ndani ya Fc Barcelona unamalizika mwakani, na hana furaha namna mambo yanavyoendeshwa klabuni hapo kwa sasa. Inter Milan wamejipanga kumsajili pindi atakapo maliza mkatba.

Nahodha wa Fc Barcelona Lionel Messi amekuwa akihusishwa kujiunga na Inter Milan ya Italia.

Inaaminika wamiliki wa Inter Milan Suning Holdings Group wameandaa bajeti ya kumnunua Lionel Messi kutoka Fc Barcelona ya Hispania atakapo maliza mkatba wake, mkataba wa sasa wa Messi unamalizika mwakani juni 30 2021.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa Messi hana furaha ndani ya Barcelona na ndio sababu inayotajwa itamfanya mchezaji huyo bora wa Dunia mara 6 asiongeze mkataba wa kuendelea kuitumikia Fc Barcelona. Ripoti mbali mbali zinasea Messi hafurahishwi namna timu hiyo inavyoendeshwa na bodi ya utendaji chini ya Rais Josep Maria Bartomeu hasa namna inavyofanya shughuli za usajili lakini pia hafurahishwi na mbinu za kocha Quique Setin.

Baada ya kufungwa na Osasuna kwenye moja ya mchezo wa Ligi kuu Hisapnia LaLiga kwa mabao 2-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbanai Camp Nou ikiwa ni kwa mara ya kwanza wanapoteza katika uwanja wao wa nyumbani toka November 2018, Messi alisema kikso chao hakipo sawa na ni dhaifu na kama watandelea kucheza kwa kiwango hicho basi hawawezi kuifunga Napoli kwenye Ligi ya mabingwa barani Ulaya yani Uefa Champions League.

Lakini pia Messi anaamini wameshindwa kutetea ubingwa wa ligu kuu Hispania LaLiga kutokana na udhaifu wa kikosi chao, hivyo waliirahisishia kazi Real Madrid kutwaa ubingwa huo. Barcelona imemaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa LaLiga kwa tofauti ya alama 5 nyuma ya mabingwa Real Madrid.

Hivyo Inter Milan wamejipanga kuinasa saini ya nahodha huyu wa timu ya taifa ya Argentina na Fc Barcelona kama hatafikia makubaliano ya kasaini mkataba mpya kutokana na makando kando yanayoendelea ndani ya Fc Barcelona.