Salehe amesema, katika mechi mbalimbali za majaribio, timu yake imeweza kufanya vizuri hivyo kujiwekea imani ya vijana wake kuwa na uwezo wa kuingia katika kikosi cha timu ya Taifa ya vijana na kuweza kufanya vizuri katika timu hiyo.
Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Kinondoni, Mwinyimadi Tambaza amesema, timu yake imecheza mechi nyingi za kirafiki japo wameshindwa kufanya vizuri kutokana na ugeni katika mechi hizo.
Tambaza amesema, vijana hao wanatakiwa maandalizi ya mapema pamoja na kambi ya muda mrefu itakayoweza kuwasaidia kuzoeana na kufanya vizuri katika mechi za kirafiki pamoja na mashindano hayo ya kitaifa.
Michuano ya kitaifa ya vijana inatarajiwa kufanyika jijini Mwanza mwishoni mwa mwezi huu kwa kushirikisha timu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa na lengo la kutafuta timu ya taifa ya vijana itakayoweza kuandaliwa kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ya nje ya nchi.