Alhamisi , 14th Oct , 2021

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amekanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, kesi yao ya rufaa dhidi ya mchezaji Bernard Morrison iliyopo CAS imefutwa kuwa si za kweli.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli (kwenye picha kubwa) na mchezaji wa zamani wa Yanga na hivi sasa anaichezea Simba, Bernard Morrison.

Badala yake Bumbuli amesema kesi yao imepangiwa tarehe nyingine baada ya tarehe ya awali kusongezwa mbele kufuatia Jaji wa kesi hiyo kuwa na majukumu mengine.

Bumbuli amesema, "Ninachofahamu mimi ni kwamba CAS wameleta barua wakatueleza kwamba, Hukumi itatoka tarehe 24 mwezi wa 10 baada ya kuwa tarehe 29 mwezi wa 9 imehairishwa kwa kuwa Jaji alikuwa na majukumu mengine".

Hii ni mara ya tatu kesi hiyo kusogezwa mbele jambo linalowafanya wafuatiliaji wa soka nchini Tanzania hususani wale wa Simba na Yanga kusalia na shauku kubwa mnoo ya kutaka kujua hukumu hasa ya kesi hiyo.

Ikimbukwe kuwa, Mwei Agosti 2020 mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana aliipelekea klabu yake aliyotoka ya Yanga kwenye kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kukataa kuwa hana mkataba na Yanga ilhali Yanga ikidai ina mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo hadi mwaka 2022.

Baad aya vuta nikuvute, Kamati hiyo iliyokuwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Elias Mwanjala iliamua kuwa mkataba wa kati ya wawili hao ulikuwepo lakini ulikuwa na mapungufu ya kimkataba hivyo kumpa ushindi Morrison na kuwa mchezaji huru wakati ambao Nyota huyo alishasaini kandarasi ya miaka 2 na Simba.

Baada ya Yanga kutorishwa na maamuzi hayo, ilipanda kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo Duniani yaani Court of Sports Abitration ‘CAS’ na kukatia rufaa hukumu hiyo.

Tokea mwishoni mwa maka 2020 kesi hiyo ipelekwe CAS imekuwa ikirushwa tarehe za mbele hadi kufikia leo Oktoba 14, 2021 na kuacha wafuatiliaji wa soka nchini kuwa na kiu zao ambazo hazijaisha na maswali tele ya njia panda kuhusu uhalali wa mkataba wa wawili hao.

Hivi sasa Bernard Morrison anaichezea klabu ya Simba tokea msimu uliopita wa mwaka 2020-21 na kufanikiwa kutwaa mataji matatu, Ligi Kuu, Kombe la FA mara mbili pamoja na kushiriki kwa uchache wakati Simba ilipotinga hatua ya Robo fainali ya Michuano ya klabu bingwa Afrika na kutolewa na Kaize Chiefs.