Kiungo wa wekundu wa msimbazi Simba, Jonas Mkude anayetuhumiwa kwa kuwa na utovu wa nidhamu klabuni kwa mara ya pili.
Taarifa ya kughairisha kusomwa kwa hukumu hiyo ilitolewa usiku wa kuamkia leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kamanda Mstaafu, Suleiman Kova kupitia taarifa ya wazi kwa umma ambayo iliwekwa kwenye ukurasa wa mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.
Taarifa kamili ya kughairishwa kwa hukumu hiyo inasomeka kama ifuatavyo;
(Taarifa kwa umma iliyotolewa na kamati ya nidhamu ya klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake kamanda Mstaafu, Suleiman Kova).
Suala la kamati hiyo kughairisha hukumu kwa kile kilichoelezwa ni kuiagiza menejimenti ya Simba kuelekezwa kumpima Afya mchezaji huyo na ripoti ikitoka ndiyo itawezesha hukumu kamili kutoka imepokelewa kwa namna tofauti na wafuatiliaji wa soka nchini wengine wakihusisha utata wa utimamu wa akili wa mchezaji huyo jambo ambalo limewacha njia panda.
Hii ni mara ya pili Mkude kufikishwa kwenye kamati ya nidhamu, kwani mwezi wa pili mwaka huu alishutumiwa na makosa mawili ya kutohudhuria semina ya wachezaji n akuchelewa kufika kambini mambo yaliyopelekea kulimwa faini ya milioni mbili ikiwa baada ya kusimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja na kupewa onyo kali la kutorudia makosa ndani ya miezi sita.