Muonekano wa Uwanja wa Gwambina uliopo Wilayani Misungwi baada ya kufanyiwa marekebisho.
Kwa mujibu wa bodi ya ligi, Mtibwa Sugar itacheza mchezo wake wa raundi ya sita Oktoba 19 mwaka huu dhidi ya Namungo kutoka mkoani Lindi .
Ikumbukwe Uwanja wa Jamhuri ulifungiwa na bodi ya ligi muda mchache baada ya mchezo wa raundi ya nne uliowakutanisha Mtibwa na Yanga baada ya kuonekana kasoro nyingi kwenye sehemu ya kuchezea na hata vyumba vya kubadilishia nguo.
Uwanja mwingine uliofungiwa ni wa Gwambina ambao baada ya kucheza dhidi ya Kagera Sugar katika raundi ya pili ulifungiwa lakini walitumia siku 14 kuufanyia marekebisho na sasa utatumika kwa mchezo wa Oktoba 15 ambapo wenyeji watakipiga dhidi ya Mtibwa Sugar.
Timu ya Biashara United haitoutumia Uwanja wake wa Karume na badala yake imehamishia mechi zake katika Uwanja wa Kaitaba uliopo Mkoani Kagera ambapo Oktoba 14 watakua wenyeji wa Ihefu kutoka Jijini Mbeya.
Klabu ya Polisi Tanzania nayo itaendelea kuutumia Uwanja wa Ushirika uliopo Kilimanjaro watakapoikaribisha Gwambina Oktoba 19 mchezo utakaochezwa saa 10:00 jioni.