Jumatano , 29th Jun , 2016

Wakala wa mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain amethibitisha kuwa nyota huyo hatorefusha mkataba wa kuendelea kuichezea klabu yake hiyo ya sasa.

Gonzalo Higuain(pichani) akishangilia moja ya bao aliloifungia Napoli.

Nicola Higuain ambaye ni kaka yake Gonzalo amesema licha ya mteja wake huyo kuwa na mkataba utakaomalizika mwaka 2018, bado anaweza kuondoka kwa ada ya pauni milioni 72.

Higuain mwenye umri wa miaka 28 alionesha umwamba wake wa kupachika mabao msimu uliopita alipofunga mabao 36 na kuipiku rekodi ya Gwiji wa zamani la klabu ya AC Milan Gunnar Nordhal .

Zipo ripoti zinazosema kuwa nyota huyo anawaniwa kwa karibu na klabu ya Atletico Madrid ya Hispania huku klabu za Arsenal na Liverpool zote za England nazo zikionesha nia ya kutaka sani ya nyota huyo.