Jumatano , 9th Sep , 2015

Chama cha Baiskeli nchini CHABATA kimesema, hakitaweza kushiriki mashindano yoyote ya kimataifa kwa mwaka huu baada ya kukosa wafadhili ambao wangeweza kuisaidia timu ya Taifa.

Makamu mwenyekiti wa CHABATA Simon Jackson amesema, baada ya timu ya taifa ya mchezo huo kuondolewa kwenye orodha ya michezo iliyotakiwa kushiriki michuano ya All Africa Games haitapata fursa nyingine kushiriki mashindano ya kimataifa mwaka huu.

Jackson amesema, chama kimekosa ufadhili hivyo kimeshindwa kuandaa kabisa kuandaa mashindano ya taifa na hakiwezi kupata nafasi yoyote ya kushiriki mashindano ya nje ya nchi.