
Kocha Msaidizi Juma Mwambusi (Katikati) Kocha Mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm (kushoto) na Kocha wa makipa Juma Pondamali
Mwambusi amesema, hawajaingia katika hatua hiyo kwa ajili ya kuangalia mashindano yapo vipi laikini wameingia kwa ajili ya kutafuta ushindi ambao utawasaidia kujiimarisha zaidi.
Mwambusi amesema, wanajua wanakutana na TP Mazembe ambayo ni timu yenye uzoefu mkubwa kuliko wao lakini na wao pia wanauzoefu kwa kuwa wameshacheza mechi na timu tofauti tofauti.
Mwambusi amesema, pamoja na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi lakini wanaamini wachezaji waliopo watafanya vizuri ili kuweza kuibuka na ushindi wa nyumbani hapo kesho.