Jumatano , 20th Jul , 2016

Kizungumkuti cha kashfa ya dawa zilizopigwa marufukua michezoni, bado kinaiweka njia panda nchi ya Urusi, na huruma ya IOC, ndiyo inasubiriwa kujua hatma ya wanariadha wake kama watashiriki mashindano ya Olimpiki.

Rais wa IOC Thomas Bach

Urusi lazima isubiri hadi maamuzi ya mwisho kujua kama wanaridha wake watashiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwezi ujao, mjini Rio.

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC), imesema itafanya maamuzi ya kisheria kabla ya kuamua kuweka adhabu ya jumla kwa wanariadha wote wa Urusi.

Pia, IOC, imesema itapima wanariadha wote wa Urusi walioshiriki, Olimpiki ya majira ya baridi mjini Sochi, 2014, kufuatia ripoti ya Dr.Richard McLaren, iliyosema zoezi la upimaji vinasaba kwa idadi kubwa ilifanyika kwenye Olimpiki ya majira ya joto na baridi, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2011 hadi Agosti 2015.