Harry Kane Mshambuliaji wa Bayern Munich jana alifunga goli tatu hat-trick dhidi ya Stuttgat na kufikisha idadi ya hat-trick Sita tangu ajiunge na Bavarians kutokea Tottenham Hotspurs ya Uingereza. Kane anashikilia rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye asili ya Uingereza aliyefunga goli nyingi zaidi kwenye ligi kuu nchini Ujerumani mbele ya Kevin Keegan, Jude Bellingham na Tony Woodcock.
Bayern Munich imefanikiwa kurudi kileleni mwa ligi kuu nchini Ujerumani mbele ya RB Leipzig kwa tofauti ya idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa. Harry Kane aliifungia timu hiyo mabingwa watetezi wa Bundesliga goli tatu ( hat-trick) na kufanya afikishe idadi ya hat-trick ya sita tangu ajiunge na kikosi hiko cha mabingwa wa kihistoria nchini Ujerumani.
Nahodha wa England ameshafunga goli Nane katika michezo Saba ya Bundesliga na kufikisha idadi ya goli 13 katika michezo 10 ya mashindano yote msimu huu wa 2024-2025. Kane anashikilia rekodi ya kufunga goli nyingi kwa Wachezaji wenye asili ya Uingereza kwenye ligi kuu nchini Uingereza amemzidi Jude Bellingham,Kevin Keegan na Tony Woodcock.
Bayen Munich imepata ushindi wa kwanza siku ya jana baada ya kucheza michezo mitatu bila matokeo ya ushindi, matokeo hayo dhidi ya Stuttgat yana umuhimu mkubwa kwa kikosi kinachonolewa na Vincent Kompany raia wa Ubeligiji kuelekea mchezo wa katikati ya wiki iajyo dhidi ya Barcelona ambao utakuwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ulikuwa mchezo mgumu kwa Bavarians dhidi ya timu inayoshika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi nchini humo, Vijana na kocha Sebastian Hoeneb waliipa mechi ngumu timu yenye masikani yake kwenye dimba la Arianz Arena na iliwachukua mpaka dakika ya 57 kupata goli la ufunguzi kupitia kwa Nahodha wa timu ya Uingereza. dakika tatu baadae Kane aliongeza goli la pili na akakamilisha goli lake la tatu kwa usiku wa jana kabla Kingsley Coman kufunga la nne lililozima ndoto za Stuttgat kurejea mchezoni.
Harry Kane anashika nafasi ya pili barani Ulaya nyuma ya Erling Haaland mwenye goli 10, Kane anamfuatia akiwa amefunga goli 8 katika ligi kuu nchini Ujerumani na kufanya mbio za mfungaji bora barani Ulaya kwa msimu wa 2024-2025 kuwa na ushindani mkubwa.