Jumatatu , 27th Oct , 2014

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope amesema suala la kusimamishwa wachezaji wa klabu hiyo Amri Kiemba, Shaban Kisiga na Haruna Chanongo ni kutokana na uchunguzi uliofanyika na kuonekana walicheza chini ya kiwango.

Akizungumza na East Africa Radio, Hanspope amesema kiwango cha mchezaji kinategemea na nafasi anayochezea, hivyo bado wanaendelea na uchunguzi ili kujua ni nini chanzo cha wachezaji hao kucheza chini ya kiwango katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu.

Hans Pope amesema mchezaji anaweza akawa na kiwango kizuri lakini tatizo likawa kwa kocha kutokana na programu anayoitumia katika mazoezi.