Jumanne , 23rd Nov , 2021

Kampuni ya GSM imeingia mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ ili kuwa wanadhamini wenza wa Ligi kuu ya NBC Tanzania, mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni mbili na milioni mia moja leo Novemba 23, 2021.

(Makamu wa Kwanza wa Rais TFF, Athuman Nyamlani (Kulia) na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Group Eng.Hersi Said (kushoto) wakionesha mfano wa Hundi ya mkataba uliosainiwa leo wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya NBC wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.1 kwa miaka 2.)

Baada ya kusaini mkabata huo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Eng. Hersi Said amesema hiyo ni juhudi ya moja kwa moja katika kuvisaidia vilabu ili view na ustawi ambao utakuza upinzani na kukuza soka nchini.

Nae, Mwakilishi wa TFF, Makamu wa kwanza wa Rais TFF, Athuman Nyamlani amewashukuru GSM kwa udhamini huo na kusema kwa hakika ni jambo jema kwenye mpira wa Tanzania.

Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu anasalia kuwa NBC, Lakini GSM ataendelea kuwa mdhamini mwenza kama ambavyo msimu uliopita walikuwa Azam na Benki ya KBC.

Baada ya malipo ya kodi serikalini na mgao wa asilimia kadhaa kwenye TFFF, asilimia kubwa ya fedha hizo zitagawanywa kwa vilabu ili kuvisaidia kuendesha shughuli zao za kila siku na hatimaye kukuza upinzani wa ligi ya NBC Tanzania.