Alhamisi , 1st Jul , 2021

Kinda wa klabu ya Chelsea Billy Gilmour anatarajia kufanya vipimo vya afya baadae leo hii katika kukamilisha  uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Norwich City kwa mkopo.

Bil Gilmour akiwa ameshika tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kati ya Scotland dhidi ya Wales alipoonesha kiwango bora.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kutumia msimu ujao akiwa na Norwich baada ya Chelsea kumpa ruhusa kiungo huyo wa Scotland kuondoka kwa msimu ujao 2021/22.

Kwa mujibu wa taarifa Gilmour atafanya vipimo vya afya leo Alhamisi mara tu baada ya kumaliza muda wake wa kukaa karantini baada kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona akiwa katika michuano ya Euro 2020.