Fury na Wilder kuzichapa tena Oktoba 9

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Pigano la tatu la uzito wa juu Duniani kati ya Tyson Fury dhidi ya Deontay Wilder limepangwa kufanyika tarehe 9 Oktoba Mwaka huu.

Tyson Fury (kulia) dhidi ya Deontay Wilder (kushoto) walipokuwa wakionyeshana ubabe kwenye pambano lililopita.

Mpambano huo, ambao ulipaswa kufanyika Las Vegas mnamo Tarehe 24 Julai, uliahirishwa baada ya Fury wa Uingereza kkukutwa na ugonjwa wa Corona.

Fury mwenye umri wa miaka 32, alimpiga Wilder mwenye umri wa miaka 35, na kuwa bingwa wa WBC mnamo Februari 2020 ikiwa ni miezi 14 baada ya miamba hao kutoka sare kwenye pigano la kusisimua huko Jijini Los Angeles.

Hakuna bondi yeyote aliyepigana tangu ushindi wa Fury huko Las Vegas.