(C.E.O wa Yanga SC, Senza Mazingiza na shambuliaji, Fiston Mayele)
Fiston Mayele ndiye kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu huu wa 2021-22 ambao bado unaendelea akiwa na mabao 14 sawa na George Mpole wa Geita Gold.
Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo amekuwa akihusishwa kujiunga na vilabu vya RS Berkane ya Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya kuvutiwa na umahiri wa kupachika mabao wa nyota huyo.
“Mayele ni mchezaji bora kinara wa ufungaji Tanzania na RS Berkane wanamtaka na klabu zingine zitamtaka. Yanga inamkataba na Fiston Mayele na unaendelea mpaka msimu ujao” Amesema Senzo
Kwa upande mwingine Senzo Mazingiza ameweka wazi kuwa kueleka kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu wa 2022-23 kikosi cha Yanga kitaundwa kumzunguka mshambuliaji huyo katika harakati za kuhakikisha wanakuwa na timu ya ushindani.
“Unaendaje kwenye michuano ya CAF na unaanza kuuza wachezaji? siwezi. Mayele haendi kokote anabaki nasi ni mchezaji wetu. Tutacheza kumzunguka yeye na kushindana klabu bingwa Afrika.” Amesema Senzo
