Alhamisi , 8th Jul , 2021

Mchezaji wa Tenisi, Roger Federer ameshindwa kuendelea na safari ya kuwania taji la 9 la Wimbledon baada ya kutupwa nje ya mashindano na Hubert Hurkacs kwa seti za moja kwa moja.

Nyota wa Tenisi kutoka Uswizi, Roger Federer akionekana kuhuzunika baada ya kupoteza mchezo.

Raia huyo wa Uswizi alipoteza kwa 6-3 7-6 (7-4) 6-0 dhidi ya mchezaji aliye katika nafasi ya 14 kwa ubora,ambaye ametinga nusu fainali yake ya kwanza ya Grand Slam na sasa atacheza dhidi ya Matteo Berrettini siku ya Jumapili.

Federer mwenye umri wa maika 39, na siku 337 alikuwa anawania kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kutinga nusu fainali ya Wimbledon katika historia ya mashindano hayo lakini imeshindikana.

Katika hatua nyingine Federer amedokeza kuwa hafahamu iwapo atashiriki michuano ijayo ya Wimbledon.

Kuondolewa kwa Federer kutanoa nafasi kubwa kwa bingwa mtetezi Novak Djokovic ambaye alimshinda Marton Fucsovics kutwaa taji la michuano hiyo na sasa ataumana na Denis Shapovalov katika hatua ya nusu fainali.