
Mwenyekiti wa CHANETA-Mama Anna Kibira.
Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira amesema kuwa, michuano ya mwaka huu ilikua na msisimko na ushindani mkubwa japo suala la kutokuwepo kwa udhamini wa jumla wa michuano hiyo, kumechangia kupunguza ushindani zaidi
Aidha Kibira amefurahishwa na ubora wa timu za wanaume katika michuano hiyo, ambayo kwa mara ya kwanza imeshirikisha timu nane za wanaume ambazo zilionyesha kiwango cha juu sana.