
Mashabiki wakiwa uwanjani
Hali hiyo inaenda sambamba na ukuaji wa ligi mbalimbali barani humo, ambapo thamani za ligi zinazidi kupaa mwaka hadi mwaka kutokana na shuguli mbalimbali ikiwemo biashara ya kuuza na kununua wachezaji, uwekezaji wa makampuni mbalimbali katika soka na shughuli nyingine.
Hizi hapa ni ligi sita zinazoongoza kwa thamani kubwa barani Afrika kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Transfer Market, ambapo ligi kuu ya soka nchini Misri 'Egyptian Premier League' imeongoza katika bara la Afrika ikiwa na thamani ya Euro milioni 149.43, ina jumla ya timu 18 na wachezaji 544.
Ligi ya pili inayofuata kwa thamani kubwa Afrika ni ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini 'ABSA Premiership', ambayo ina thamani ya Euro milioni 147.20, ikiwa na jumla ya timu 16 na idadi ya wachezaji wanaocheza ni 557. Ligi ya tatu kwa thamani ni ligi kuu ya soka nchini Morocco 'Botola Pro League', yenye thamani ya Euro milioni 131, idadi ya timu 16 na jumla ya wachezaji 433.
Namba nne inashikiliwa na ligi kuu ya soka ya Tunisia 'Ligue I Pro' yenye thamani ya Euro milioni 109.80, idadi ya timu 16 pamoja na jumla ya wachezaji 464, huku ligi kuu ya soka nchini Algeria ikishika namba tano, ikiwa na thamani ya Euro milioni 88.63 na idadi ya timu ikiwa ni 16 pamoja na jumla ya wachezaji 446.
Ligi kuu ya soka nchini Nigeria inashika namba sita kuwa na thamani kubwa Afrika, ambapo Euro milioni 12 imewekezwa, idadi ya timu ikiwa ni 25 na wachezaji wanaocheza ligi hiyo ni 758.