Eng.Hersi Said upande wa kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Yanga Dr.Mshindo Msola.
Eng.Hersi ameandika kwenye ukarasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagramm. Nguzo tatu za mafanikio katika timu ya mpira wa miguu,1)Uongozi bora, 2)Idara bora ya ufundi, 3)Wachezaji wadaraja la juu.
Akamalizia kwa kusisitiza ‘Katika kufikia malengo yetu, tunalazimika kujenga maeneo haya matatu kwa UMAKINI, UWELEDI, UZALENDO na MAPENZI MEMA kwa klabu yetu. AIDHA, ujenzi huu utafanyika katika muda mfupi tulionao bila kusita wala kutetereka. HESABU SIKU KUANZIA SASA KATIKA SAFARI HII itakayo wavutia sasa na hata vizazi vyetu hapo kesho’. Amandika Eng. Hersi.