Jumatano , 2nd Apr , 2014

Mpiganaji wa sanaa ya mapigano ya mashariki ya mbali yaani Martial Arts aina Muai Thai na Mixed Martial Arts (MMA) mtanzania Emmanuel Shija Kajala amesema hivi karibuni ataenda nchini Hispania kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kwa mchezo huo.

Emmanuel Shija kabla ya kupanda ulingoni huko India,Muay Thai Style Club

Emmanuel Shija ambaye ameshiriki mashindano mbali mbali duniani amesema ameweza kufanikiwa kimataifa kutokana na mafunzo aliyoyapitia katika nchi mbalimbali duniani ambako alitunukiwa vyeti baada ya kuhitimu.

Shija amesema amezunguka mabara yote duniani akicheza mchezo huo na mwaka 2012 alishiriki Tamasha la Amani na Michezo mjini Tehran lililoandaliwa na serikali ya Irani chini ya Rais mstaafu wa nchi hiyo mheshimiwa Mahmoud Ahmadinejad.