Djokovic, Nadal kuminyana nusu fainali French Open

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Mcheza tennis namba moja Novak Djokovic raia wa Sebia ataminyana na Rafael Nadal wa Hispania kwenye mchezo wa nusu fainli ya michuano ya wazi ya Ufaransa, baada ya wote wawaili kushinda micho ya robo fainali jana usiku.

Novak Djokovic wa kushoto, akiwa na Rafael Nadal

Djokovic mshindi wa michuano hii mara moja mwaka 2016 amefuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3-1 ( 6-3 6-2 6-7 (5-7) 7-5) dhidi ya Matteo Berretini raia wa Italia. Sasa katika hatua ya Nusu fainali Djkovic atakutana na Rafael Nadal ambaye ni bingwa mara 13 wa michuano hii.

Nadal ambaye ni mchezaji namba tatu kwa ubora ametinga nusu fainali baada ya kumfunga Diego Schwartzman raia wa Argentina kwa ushindi wa seti 3-1, (6-3 4-6 6-4 6-0 ), ni kwa mara ya 14 Nadal raia wa Hispania anatingwa hatua ya nusu fainali ya French Open lakini pia akiwa anauwinda ubingwa wa 14.

Wawili hawa watakuwa wakikutana kwa mara ya 58, Djokovic akiwa ameshinda mara nyingi zaidi mara 29 wakati Nadal ameshinda mara 28.

Mshindi wa mchezo huu wa busu fainali atakutana na mshindi wa mchezo mwingine wa nusu fainali ambao unawakutanisha Stefanos Tsitsipas raia wa Ugiriki dhidi ya mjerumani Alexander Zverev.