Jumatatu , 13th Nov , 2023

Novak Djokovic amejihakikishia kumaliza nafsi ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa wachezaji wa tenisi Dunia upande wa wanaume mwaka 2023. Djkovic anamaliza mwaka akiwa namba 1 baada kushinda jana usiku dhidi ya Holger Rune.

Novak Djkovic atamaliza mwaka 2023 akiwa mchezaji namba 1 kwa ubora Duniani upande wa wanaume.

Djokovic alihitaji ushindi kwenye mchezo mmoja tu ili kujihakikishia kumaliza akiwa mchezaji kinara (namba 1) kwa mwaka 2023 baada ya kumfunga Holger Rune kwenye mchezo wa ATP Tour wa Turini huko Italia.

Djokovic ameshinda kwa set 2-1 yani 7-6, 6-7 na 6-3. Mchezo uliochezwa masaa3 na dakika 4. Ni mwaka wa 8 tofauti Novac Djkovic raia wa Serbia anamaliza akiwa nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa tenisi upande wa wanaume.

Ndani ya mwaka huu 2023 Djkovic mwenye miaka 36 ameshinda mataji 6 na anaiwinda rekodi ya mataji 7 ndani ya mwaka 1 endapo kama atashibda ubingwa wa Turin. Mataji aliyoshinda mwaka huu ni Cincinnati Masters, Adelaide International, Paris Masters, US Open, French Open na Australian Open.