Alhamisi , 19th Dec , 2024

Golikipa wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Mali Djigui Diarra atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita akiuguza majeraha ya kigimbi cha mguu na nyama za paja.

Diarra atakosa michezo ya ligi kuu kuu Tanzania bara pamoja na ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Januari 3, Al Hilal januari 10, na MC Algers utakaochezwa Januari 17 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Golikipa wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Mali Djigui Diarra atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita akiuguza majeraha ya kigimbi cha mguu na nyama za paja.

Taarifa za Dakatari wa timu hiyo Moses Etutu amelishauri benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Sead Ramovic kumuacha Mchezaji huyo apone kabisa kwakuwa wakimuwaisha kurudi uwanjani kunaweza kumsababishia matatizo makubwa zaidi.

Diarra atakosa michezo ya ligi kuu kuu Tanzania bara pamoja na ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Januari 3, Al Hilal januari 10, na MC Algers utakaochezwa Januari 17 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Yanga SC imesaliwa na Magolikipa wawili kikosi cha kwanza Aboubakar Khomeni na Abuutwalibu Mshery mpaka pale Diarra atakaporejea uwanjani.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Mali atakuwa pengo kubwa kwa Mwalimu Sead Ramovic kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuondoa hatari langoni mwake,kupanga vizuri safu yake ya ulinzi pamoja na kuanzisha mashambulizi.

Djigui Diarra ni mmoja wa Magolikipa bora Afrika wanaocheza ligi kuu Tanzania bara kukosekana kwake kutaiathiri timu ya Yanga kwa namna moja au nyingine haswa kwenye michezo ya ligi ya mabingwa Afrika.

Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu bara kinaendelea na jitihada zake za kurudi kwenye ubora wake baada ya kupitia kipindi kigumu kutokana na kupata matokeo mabaya mfululizo.