Jumatano , 22nd Jun , 2022

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limetoa taarifa rasmi ya dirisha kubwa la usajili kwa vilabu vinavyo shiriki ligi zote zilizopo chini ya shirikisho hilo la soka nchini Tanzania.

Nembo ya shirikisho la soka Tanzania TFF

Taarifa hiyo itavihusu vilabu vyote vinavyoshirki ligi kuu ya NBC Tanzania bara,ligi daraja la kwanza (Championship), ligi daraja la pili ( First League) na ligi kuu ya wanawake Tanzania bara Serengeti Lite msimu wa mwaka 2022/ 2023. Dirisha hilo la usajili litafunguliwa rasmi tarehe 1 Julai 2022, na litafungwa tarehe 31 mwezi Agosti mwaka 2022.

Katika kipindi hicho pekee vilabu vyote vinatakiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wote kwa wakati, pamoja na uhamisho wa wachezaji wa kimataifa. Vilabuvyote vinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili ulioidhinishwa sababu hakuta na muda wa ziada baada ya dirisha hilo la usajili kufungwa.

Pia shirikisho hilo la soka Tanzania limesisitiza kwamba klabu yoyote atakayekutana na changamoto awasiliane na idara ya mawasiliano ya TFF. Aidha taarifa hiyo pia imeeleza kuhusu dirisha dogo la usajili kwamba litafunguliwa tarehe 16 Desemba 2022, na litafungwa tarehe 15 Januari 2023.