Nahodha wa zamani wa Uruguay na Mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England atashiriki mashindano ya Tennis yatakayofanyika Uruguay Montevideo. Forlan ana umri wa miaka 45 atashirikiana na Federico Coria kwenye michezo ya wawili kwa wawili.
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uruguay na klabu ya Manchester United atashiriki kwenye mashindano ya Tennis ya ATP yatakayofanyika Montevideo nchini Uruguay. Forlan atashirikiana na nyota wa Argentina Federico Coria katika michezo ya wawili kwa wawili.
Nahodha huyo wa zamani wa Uruguay aliwahi kucheza Tennis akiwa kijana mdogo na alikuwa mchezaji mzuri wa mchezo huo kabla ya kuchagua kucheza mpira wa miguu. kwa sasa Forlan anashika nafasi ya 108 kwenye orodha ya Wacheza Tennis wenye miaka 45 na zaidi Duniani.
Michezo ya ATP ya Montevideo inatarajiwa kuanza kufanyika mwezi Novemba 2024, Mshindi wa mpira wa Dhahabu kwenye fainali za kombe la Dunia lililofanyika Afrika ya Kusini mwaka 2010 anatizamwa kama kivutio kutokana na mafaniko yake aliyoyapata kwenye mpira wa miguu na kuwashangaza watu wengi kwa kuhamia kwenye mchezo wa Tennis.
Diego Forlan aliwahi kutamba na klabu za Villarreal, Atletico Madrid za nchini Hispania kabla kwenda kucheza India alipata umaarufu sana enzi za uchezaji wake kutokana na utaalamu wake mkubwa kwa kupiga mipira ya adhabu kwa kutumia mipira ya Jabulani ambayo iliwashinda Magolikipa wengi nchini Afrika ya Kusini.
Tangu astaafu kucheza mpira wa miguu mwaka 2018, amekuwa akifanyia mazoezi mchezo wa Tennis na ameshiriki kwenye mashindano ya Shirikisho la Tennis Duniani ITF mwaka 2023, anaungana na Wacheza mpira wengine kama Eric Cantona, Petr Cech, Jens Dudek na Gabriel Batistuta waliochagua kuhamia kucheza michezo mingine baada ya kustaafu mpira wa miguu.