Alhamisi , 10th Sep , 2015

Mashindano ya mchezo wa kurusha vishale ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kuanza Septemba 25 hadi 28 mwaka huu jijini Arusha.

Katibu mipango wa chama cha mchezo wa vishale mkoani Dar es salaam Kamdasi Kibago amesema, nchi zote za Afrika Mashariki zimethibitisha ushiriki wa mashindano hayo na zitatakiwa kufika siku moja kabla ya mashindano.

Kibago amesema, mashindano hayo yatakuwa ya wazi hivyo kila nchi itawakilishwa na timu nyingi kadri itakavyoweza kuwahudumia wachezaji wake katika siku zote za mashindano hayo.

Kibago amesema, mpaka sasa bado haijajulikana Tanzania itawakilishwa na timu ngapi lakini kila moa umetakiwa kujiandaa na mashindano hayo hivyo kuna uwezekano mikoa yote inayocheza mchezo huo ikashiriki.