Crystal Palace waachana na Nuno Espirito Santo

Jumatano , 9th Jun , 2021

Klabu ya Crystal Palace imesitisha mazungumzo na aliyekua kocha wa wolves Nuno Espirito Santo kwa sababu ya madai kwamba wakuu wa kilabu hiyo wana wasiwasi ba kocha huyo mreno, na juu ya kuonesha mapenzi yake kwa klabu ys Everton.

Kocha Nuno Espirito Santo

Crystal Palace wameamua kuachana na harakati za kumnasa kocha Nuno baada ya Maafisa wa Crystal Palace kukutana Jumanne usiku na kuafikiana kufuta zoezi hilo. Santo alitoa mahitaji yake kadhaa ya kimaslahi na Palace wakaamua kuangalia upande wa maslahi yao zaidi.

Wakati huo klabu ya Wolves imethibitisha Bruno Lage kua kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu na mkufunzi huyo wa zamani wa Benfica amekiri kwamba anataka kuboresha kazi ya mtangulizi wake aliyeondoka.