Ijumaa , 13th Mei , 2022

Vilabu vya Chelsea na Liverpool watakuatana kwenye mchezo fainali ya kombe la FA jumamosi hii Mei 14, 2022 ikiwa ni mara ya pili kwa timu hizi kukutana kwenye hatua ya fainali msimu huu baada ya kukutana kwenye faini ya Carling Cup mwezi February mwaka huu.

(Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel)

Kuelekea mchezo huu wa fainali kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa watakosa huduma kiungo wao Farbinho anayesumbuliwa na maumivu ya misuli huku Chelsea nao wakiwakosa nyota wao kadhaa akiwemo mlinzi Ben Chillwell, Hodson Odoi na Mateo Kovacic wanaosumbuliwa na Majereha.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Wembley majira ya saa 12 na dakika 45 jioni kwa saa za Africa Mashariki. Na kwa upande wa kocha wa timu ya taifa ya England Gareth South Gate atakua na nafasi nzuri ya kuangalia maeneo machache ya timu ya taifa ya England ambayo yatampa Gareth Southgate machaguo mengi zaidi kuelekea Kombe la Dunia hasa katika upande wa mlinzi wa kulia.

Kocha huyo wa Three Lions ana idadi kubwa ya chaguzi ambapo kuna Kyle Walker wa Manchester City, Kieran Trippier wa Newcastle, Trent Alexander-Arnold wa Liverpool na Reece James wa Chelsea, lakini Trend Alexander-Arnold na Reece James ndio wamekuwa na msimu mzuri safari hii