Pambano hilo limeandaliwa kwa lengo la kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka amesema ameaua kumtuafutia mpinzani wa nje bondia wake kwa lengo la kumpandisha kiwango ili aweze kucheza mapambano makubwa duniani.
Ndabile amesema ameamua kuondokana na kuwaandalia mabondia wake mapambano dhidi ya mabondia wa hapa hapa kwani hawapati uzoefu wa kimataifa.
Kwa upande wake, Cheka amesema amejiandaa vyema kwa pambano hilo na anataka kuonyesha ubora wake katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Cheka amesema anatarajia kushinda katika pambano hilo ili kuendeleza rekodi yake katika ngumi za kulipwa.
Cheka amesema Moliyati ni bondia mzuri na anajua atampa upinzani mkali, lakini hatokubali kupoteza katika ardhi ya Tanzania kwani amejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo.
Mbali ya mapambano hayo, pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia nyota, Japhet Kaseba atawania ubingwa wa Taifa wa TPBC Limited dhidi ya bondia nyota kutoka Zanzibar, Amour Mzungu katika pambano la uzito wa juu, huku Alphonce Mchumiatumbo akizipiga na bondia Mussa Ajibu kutoka Malawi katika pambano la uzito wa juu kabla ya Ashraf Suleiman kuonyeshana kazi na Aliki Gogodo wa Malawi katika pambano la uzito wa juu pia.
Pambano lingine la ubingwa litakuwa kati ya bondia Shabani Kaoneka dhidi ya Zumba Kukwe la uzito wa middle raundi 10 ambapo Yonas Segu atazichapa na bondia wa Malawi, Wilson Masamba katika pambano la uzito wa Light-Welter la raundi nane.
Mabondia wa kike, Lulu Kayage atazichapa na Enelesi Nkwanthi katika pambano la uzito wa bantam la raundi sita.