Jumatano , 3rd Jun , 2015

Bondia wa Ngumi za Kulipwa nchini Francis Cheka amechumpa katika viwango vya ubora wa ngumi Duniani kutoka nafasi ya 56 mpaka ya 41 mara baada ya kumtandika Bondia mthailand, Kiatchai Singwancha kwa TKO raundi ya nane mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika taarifa yake, katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa Antony Rutta amesema, ushindi wa Cheka dhidi ya Bondia huyo umeiletea heshima Tanzania na kuipandisha katika ubora wa kimataifa.

Rutta amesema, kutokana na ushindi huo, cheka atapigana na bondia mwingine kutoka nchini Iran ambaye bado jina lake halijajulikana.

Kwa upande wake Cheka amesema, lengo lake ni kuhakikisha siku moja anakuwa bingwa wa dunia kupitia mchezo huo hivyo ataendelea kujifua ili aendelee kuipa heshima nchi yake.