Ijumaa , 20th Nov , 2015

Michuano ya Kombe la CECAFA Chalenji inaanza kutimua vumbi hapo kesho nchini Ethiopia kwa kushirikisha nchi 11 ambapo timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imepangwa kundi moja na wenyeji Ethiopiakatika michuano hiyo mwaka huu.

Michuano hiyo itazinduliwa rasmi hapo kesho kwa kuchezwa mchezo wa kundi B kati ya Burundi na Zanzibar Heroes kutoka visiwani Zanzibar ikifuatiwa na mchezo wa kundi A kati ya mwenyeji wa michuano hiyo Ethiopia dhidi ya Rwanda.

Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi hapo Jumapili ambapo timu za kundi A The Kilimanjaro Stars ya Tanzania itamenyana na Somalia huku ukifuatiwa na mchezo wa kundi B kati ya Kenya na Uganda.