Jumapili , 20th Apr , 2014

Vijana wametakiwa kujitokeza kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na michezo ya Baiskeli hali itakayowasaidia kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es salaam,Suleiman Kova.

Vijana wametakiwa kujitokeza kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na michezo ya Baiskeli hali itakayowasaidia kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Akiongea Mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya muungano katika mbio za baiskeli za kilomita 100 yaliyoanzia Mwenge kuelekea Tandika na kumalizuia fukwe za Coco,Kamishna wa Polisi kamanda maalum ya Dar es salam,Suleimani kova amesema vijana wasijikite katika mpira wa miguu badala yake washiriki katika michezo mingine.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo kutoka wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo ,Juliana Yasoda amesema vijana wauthamini mchezo huo kwani utaweza kuwaletea mafinikio makubwa ikiwa ni pamoja na medali mbalimbali Kama endapo watafanikiwa kushiriki katika michuano ya Olimpiki.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Tanzania CHABATA,Godfrey Muhagama amesema wachezaji 24 walioshiriki mashindano hayo wakiwemo wa timu ya taifa waendelee kuonyesha ushindani ili waendelee kuwepo katika timu hiyo kuelekea katika mashindano ya kimataifa.