
Mlinda mlango wa Chelsea, Petr Cech kabla ya kutundika daruga.
Cech mwenye umri wa miaka 38 amejumuishwa kwenye kikosi hicho kama mchezaji huru na anaingia kikosini kama mchezaji wa dharula.
Mlinda mlango huyo alistaafu kucheza soka mwaka 2019, kwasasa ni mshauri wa ufundi na utendaji wa klabu ya Chelsea.
Kujumuishwa kwa Cech imeelezwa kama hatua ya tahadhari kutokana na hali ambazo hazijawahi kutokea kwasasa zinazosababishwa na mzozo wa Covid-19.
Alicheza zaidi ya michezo 300 tangu msimu wa 2004 hadi 2015 akishinda mataji makubwa 13 yakiwemo ya ligi kuu manne, FA manne na la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2012 kabla ya kujiunga Arsenal.
Walinda mlango wengine waliopo kikosini ni pamoja na Eduardo Mendy, kepa Arrizabalaga na Willy Caballero.