Jumatano , 21st Jul , 2021

Baada ya miaka 50, hatimaye timu ya Milwaukee Bucks imeshinda ubingwa wa ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA baada ya kuibuka na ushindi wa alama 105 kwa 98 dhidi ya Phoenix Suns kwenye mchezo wa sita wa fainali uliochezwa alfajiri ya leo.

Wachezaji wa Milwaukee Bucks wakishangilia ubingwa

Bucks wanatwaa ubingwa huu baada ya kushindi mchezo wa nne kati ya sita iliyochezwa kwenye mfululizo wa michezo 7 iliyopaswa kuchezwa ya fainali ambapo Phoenix Suns wameshinda michezo miwili tu kati ya sita, Mara ya mwisho timu hiyo kutwaa ubingwa wa NBA ilikuwa mwaka 1971.

Mchezaji nyota wa timu hiyo Giannis Antetokounmpo ameibuka kuwa mchezaji bora wa fainali baada ya kufunga alama 50, mipira iliyorudi (rebounds) 14 na akitoa usaidizi wa pasi za kufunga (assists) 2, na Khris Middleton nae amefunga alama 17 na ametoa pasi za usaidizi wa kufunga 5.

Kwa upande wa Phoenix Suns ambao hawajawahi kutwaa ubingwa wa NBA wanapaswa kusubiri tena lakini mchezaji nyina na mkongwe Chris Paul kwenye mchezo wa leo amefunga jumla ya alama 26 na pasi za kufunga (assists) 5 na mchezaji mwenzake Devin Booker amefunga alama 19 , na pasi za kufunga 5.