Jumatatu , 14th Jun , 2021

Timu ya Brooklyn Nets imepata pigo lingine kubwa baada ya mchezaji wake nyota Kyrie Irving kupata maumivu ya kifundo chake cha mguu yaliyotokea baada ya nyota huyo kudondokea kifundo hicho alipojaribu kuruka na kufunga mbele ya Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee Bucks.

Kyrie Irving akiwa anaugulia baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kuamkia usiku wa jana.

Irving aliumia dakika tano za mwanzo na kuondoka uwanjani kwenda kupata matibabu jambo lililopelekea atimu yake kukosa huduma yake na kufungwa kwa alama 107-96 usiku wa kuamkia jana kwenye mchezo wa mzunguko wa nne wa nusu fainali ya NBA kwa ukanda wa Mashariki.

Alipohujiwa kuhusu hali ya nota huyo na uwezekano wa kurejea kikosini haraka kuelekea mzunguko wa tano, Kocha wa Nets Steve Nash amesema bado haijafahamika japo imeonekana maumivu hayo si makubwa sana huenda James Harden na Kyrie Irving kurejea dimbani.

Ikumbukwe kuwa utatu mtakatifu wa Nets yaani, Kevin Durrant, Kyrie Irving na James Hardenwamecheza michezo isiyozidi 9 kwa pamoja kikosini kwenye michezo ya msimu wa kawaida ya ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA'

Nets watarudiana na Milwaukee Bucks saa 11 Alfajiri ya kuamkia kesho kutwa Juni 16, 2021 wakati Atalanta Hawks watakipiga na Philadelphia 76ers saa 8:30 usiku huku Utah Jazz watakipiga na Los Angeles Lakers saa 11 Alfajiri ya kuamkia kesho Juni 15, 2021.