
Bossou hakuondoka na Yanga Dar es Salaam Alfajiri ya jana kutokana kuchelewa kurejea nchini baada ya mapumziko kwa sababu ya kile alichoripoti, matatizo ya kifamilia.
Na awali ilikuwa beki huyo aungane na timu moja kwa moja Algeria baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia, lakini sasa ataiwahi kambi ya Uturuki hataiwahi.
Yanga pia itamkosa beki wake tegemeo wa kulia, Abdul aliyeumia kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mei 25 mwaka huu Yanga ikishinda 3-1 na akaenda kujitonesha akiichezea timu ya taifa, Taifa Stars ikifungwa 2-0 na Misri Juni 4, mwaka huu.
Na kwa sababu hiyo, Juma Abdul anatakiwa kuwa nje kwa wiki mbili, hivyo beki mpya, Hassan Kessy anaweza kuanza mapema kuteleza upande wa kulia baada ya kusajiliwa mwezi uliopita kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
Mbali na Juma Abdul, wengine walioachwa ni Malimi Busungu, kipa Benedictor Tinocco na mshambuliaji Paul Nonga ambao hawamo kwenye programu ya kocha, wakati kinda Yussuf Mhilu hatakwenda kwa sababu jina lake halijasajiliwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' amesafiri lakini hatacheza mechi hiyo ya kwanza ya Kundi A kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, aliyopewa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Sagrada Esperanca nchini Angola.
Kiungo Salum Telela ni mchezaji pekee aliyemaliza msimu na Yanga ambaye hatasafiri, kwa sababu hajapewa Mkataba mpya baada ya kumaliza wa awali.
Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco, Bouchaib El Ahrach akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk.
Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika mchezo wake wa pili wa Kundi A.
Kikosi kamili cha Yanga kinachokwenda Uturuki ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
Mabeki ni Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Viungo ni Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.
Washambuliaji ni Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Msafara umeongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.