Alhamisi , 13th Jun , 2024

Boston Celtics wanaukaribia ubingwa wa 18 wa Ligi ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) baada ya kushinda mchezo wa 3 mfululizo wa fainali ya NBA kwenye mfululizo wa michezo 7 ya fainali.

Boston wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa baada ya kuinyuka Dallas Mavericks kwa ushindi wa alama 106 kwa 99 kwenye mchezo wa 3 wa fainali na kuwafanya kuongoza 3-0 kwenye mfululizo wa miichezo 7 ya fainali.

 

Nyota wa Celtics Jaylen Brown  amefunga alama 30 ribaundi 8 na pasi za usaidizi wa kufunga 8 huku Jayson Tatum amefunga alama 30 ribaundi 6 na pasi za usaidizi wa kufunga 5 huku Nyota wa Mavericks  Kyrie Irving  akifunga alama nyingi zaidi alama 35 kwenye mchezo huu lakini haikutosha kuipa ushindi Mavericks.

 

Boston Celtics mabingwa mara 17 wa NBA wanahitaji ushindi kwenye mchezo mmoja kati ya michezo 4 ya fainali iliyosalia ili kutwaa ubingwa wao wa kwanza tangu mwaka 2008.