Jumamosi , 10th Jul , 2021

Klabu ya Simba inatajwa kuwa na safu hatari ya ushambuliaji Tanzania bara kwa ushahidi wa takwimu za upachikaji mabao kwenye Ligi kuu Tanzania bara lakini takwimu za wachezaji wao wanaocheza kwenye safu hiyo zinaonyesha uwezo wa kikosi hicho kwenye upachikaji mabao.

Washambuliaji watatu wa Simba wamefunga mabao 37 wote kwa pamoja

Simba ndio timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi msimu huu kweney Ligi Kuu bara tukiwa tunaelekea mwishoni mwa msimu, ambapo mpaka sasa timu hiyo imefunga jumla ya mabao 71 ikiwa ni mabao 21 zaidi ya timu inayofatia kwenye orodha ya timu zilizofunga mabao mengi msimu huu 2020-21 wa VPL, Yanga ndiyo inashika nafasi ya pili ikiwa imefunga mabao 50.

Mabingwa hao wa Tanzania bara na vinara wa ligi wakiwa na alama 76, wamefunga mabao hayo katika michezo 31 ambao ni wastani wa kufunga mabao 2.290.. Kwa mchezo ambao ni wastani mkubwa kuliko timu zote kwani watani zao Yanga wastani wao wa kufunga goli kwa mchezo ni 1.5625 wanashika nafasi ya pili Azam wanashika nafasi ya tatu wastani wao ni goli 1.5 kwa mchezo ambapo wamefunga mabao 48 kwenye michezo 32.

Wachezaji wa Simba 

Kubwa zaidi washambuliaji watatu wa Simba wamefunga mabao kumi na zaidi yani (10+), washambuliaji hao ni John Bocco ambaye kafunga mabao 14, Chris Mugalu kafunga mabao 12 na Meddie Kagere kafumania nyavu za timu pinzani mara 11, hivyo washambuliaji hawa watatu wote kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 37 ambayo ni nusu ya mabao 71 yaliyofungwa na timu nzima ya Simba.

Mabao 37 waliofunga John Bocco, Kagere na Mugalu kwenye Ligi ni mengi zaidi kuliko magoli yaliyofungwa na baadhi ya timu za Ligi kuu, kwa mujibu wa tawaimu idadai hiyo ya mabao wamezizidi timu 15 ukitoa Yanga waliofunga mabao 50 na Azam FC mabao 48.

Ukitoa Simba, Yanga na Azam timu nyingine zilizofunga mabao yanayofika 30 ni KMC waliofunga mabao 33, Kagera Suga na Ruvu shooting zimefunga mabao 32 kila moja na JKT Tanzania amabao wamefunga mabao 30, timu nyingine zilizobaki zote zimefunga bao chini ya 30.