Jumatatu , 6th Dec , 2021

Mashindano ya mbio za magari ya Langa Langa yanayotaraji kufanyika Disemba 12 mwaka huu nchini Abu Dhabi yanataraji kuwa yenye upinzani mkali kwani yamebeba hatma ya kuamua bingwa kati ya Lewis Hamilton na Max Verstappen.

(Lewis Hamilton (kushoto) na Max Verstappen (kulia)

Wawili hao wote wana walama 369.5 baada ya Lewis Hamilton kushinda usiku wa kuamkia leo kwenye mashindano ya mbio za magari ya Saudi Arabian Grand Prix huku Verstappen akishika nafasi ya pili.

Mbio hizo ambazo zimefanyika Saudi Arabia kwa mara ya kwanza, yangetoa hatma ya bingwa wa jumla wa kalenda ya mashindano hayo kama dereva Verstappen kutoka kambi ya Redbull angeibuka kidedea mbele ya Hamilton wa kambi ya Mercedes Benz kufuatia Verstappen kuwa mbele kwa alama 8.

Ikumbukwe, Hamiliton ni bingwa mara 7 wa Dunia lakini pia ni bingwa mtetezi wa misimu minne mfululizo na kama akiwa mshindi basi ataweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi, wakati Max Varsterppen anauwinda ushindi wake wa kwanza.