Alhamisi , 17th Sep , 2015

Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania BFT limesema, kushindwa kwa wanamichezo mbalimbali ikiwemo kwa upande wa mabondia imechangiwa na kupeleka wanamichezo wachache katika mashindano ya All African Games.

Katibu mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema, nchini inapokuwa imepeleka wanamichezo wengi inakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali kwani hata kama wengine watakuwa wametoka itajiwekea imani kwa watakaokuwa wamebaki.

Mashaga amesema, "katika michezo pia inategemea na bahati pamoja na maandalizi ya mpinzani wako kama kajiandaa kwa kiwango cha juu au kiwango cha chini hivyo unakuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwa kuangalia kiwango cha mpinzani wako."

Mashaga amesema, suala la kupeleka wanamichezo wachache ni moja ya sababu itakayochangia Tanzania isiweze kupata medali katika mashindano mengi.