
Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam BD kimelazimika kufuta michuano ya ligi ya mkoa RBA kutokana na kalenda yao kuingiliana na michuano ya taifa ambayo inasimamiwa na shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF
Kaimu rais wa BD Richard Jules amesema kuwa kutokana na maamuzi hayo ya BD sasa ni wakati wa vilabu vya wilaya za Kinondoni na Ilala kushiriki kwa wingi katika ligi za wilaya hizo ili kupata wawakilishi wanne wanne watakaoungana na wanne wengine toka Temeke ilikucheza ligi ndogo ya mtoano kupata timu bora zitakazoshiriki ligi ya taifa ambayo itakuwa ni ya wazi
Amesema kuwa Temeke tayari ilishafanya mashindano ya ligi yao na washindi wanne kupatikana na sasa wanangoja washindi wa ligi za Kinondoni na Ilala ili kucheza play off kupata wawakilishi wa michuano ya taifa itakayoanza April mwanzoni.