
Nyota wa tennis Iga Swiatek
Swiatek mwenye umri wa miaka 20 ambaye kwa sasa anakamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya ubora duniani kwa upande wa wanawake na kuwa Mpoland wa kwanza kukamata nafasi ya hiyo ya juu duniani kwa viwango vya tennis.
"nililia kwa dakika 40 sababu sikujua kwa nini Ashleigh Barty ameamua kujiuzulu mana sikujua kama ni kitendo ambacho kingeweza kutokea mapema ilinishangaza sana . Siku zote nilikuwa na mawazo ya sisi wote kushindana mpaka tukifikisha miaka 35 na kuendelea lakini kwa sasa haiwezekani tena “ amesema Swiatek
Mpaka sasa Swiatek amecheza michezo 17 bila ya kupoteza huku akishindi mataji matatu ya WTA kwa mwaka 2022 huku akiingia kwenye rekodi za kuwa mchezaji wa nne kutwaa mataji mawili ya Indian Wells na Miami Open kwenye rekodi za mashindano hayo huku akichukua nafasi ya kwanza kwa viwango vya tennis akichukua nafasi ya Ashleigh Barty aliyejiuzulu kucheza mchezo huo .