Alhamisi , 31st Dec , 2015

Klabu ya Barcelona imeweka rekodi mpya kwenye ligi kuu ya soka nchini Hispania baada ya kuwapiku mahasimu wao Real Madrid kwa kufikisha mabao 180 kwa mwaka baada ya hapo jana kuicharaza Real Betis bao 4-0 kwenye mchezo wa la liga.

Barcelona wanaipiku Real Madrid kwa mabao mawili zaidi ambapo wao walifunga mabao 178 mwaka 2014.

Akiwa anatimiza mechi yake ya 500 Msahmbuliaji Lionel Messi aliifungia Barcelona bao la 425 huku Luis Suarez akifunga mawili na jingine likiwa ni la kujifunga kwa Real Betis.

Ushindi huo unawarejesha Barcelona kileleni mwa La Liga ligi kwa kufikisha pointi 38 sawa na Atletico Madrid ambayo nayo imechomoza na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Rayo Vallecano,huku Real Madrid ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 36 baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Sociedad.